DIOCESE OF MBEYA
PANDAHILL SECONDARY SCHOOL
TEL NO: +255755427518/ +255754459201 P.O. BOX 6233
MBEYA.
FAX NO: +0736607564 TANZANIA.
E-Mail:
Website: www.pandahill.org
KWA MZAZI/MLEZI WA …………………………………………….………………… ALIYECHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI PANDAHILL
Awali ya yote napenda kukupongeza mzazi/ mlezi kwa kuchagua pandahilll kuwa sehemu ya historia ya mwanao. Sisi kama shule twasema ahsante sana.
Kitaaluma; Shule yetu ya Pandahill inatilia sana mkazo katika suala zima la taaluma. Kwa hiyo basi, sera mojawapo ya shule ni kuhusu “pass mark” kwa mfano kutoka kidato cha tano kwenda cha sita mwanafunzi anatakiwa kupata angalau wastani wa asilimia hamsini (50%) au Division II point 12. Chini ya asilimia hii mwanafunzi harusiwi kuingia kidato kinachofuata. Suala hili, tunapenda liwe wazi kwa mzazi na mtoto anayependa kujiunga nasisi kwani pia lina uhusiano mkubwa na mkataba ulioambatanishwa na fomu hii. Tunaamini kiwango 50% kipo katika uwezo wa mwanafunzi yeyote aliye na bidii na mwenye kushirikisha walimu wake hasa pale anapokwama. Kwahiyo, tunatarajia mwanao atatupa ushirikiano mzuri.
Kinidhamu; Tunatilia mkazo sana sheria za shule tukiwa na matumaini kwamba zinaishika na ndizo chachu na ufunguo wa mafanikio ya mwanafunzi na shule kwa ujumla. Kwa hiyo tungependa mwanafunzi na mzazi/mlezi wazisome na kuzielewa.
Usafiri: Kwa wale watokao Dar es salaam, kwa usafiri wa barabara – tunatumia mabasi ya Kampuni ya NEW FORCE. Utaratibu ni kwenda kukata tiketi ya tarehe utakayosafiri. Hatahivyo mzazi anaweza kutumia usafiri tofauti eg. Makampuni mengine, Usafiri binafsi toa taarifa shuleni. Pia mzazi waweza tumia usafiri wa ndege. Kufungua ni tarehe 16/06/2016.
Kufunga: Siku ya kufunga shule, shule ina utaratibu wa kuwakatia tiketi wale wa mbali mfano Sumbawanga, Mpanda, Songea, Iringa, Makambako, Njombe, Morogoro, Dodoma, Dar es salaam etc. wale wa Mbeya au wanaotoka maeneo ya karibu na shule: huenda wenyewe nyumbani, wengine wazazi huwafuata hapa shuleni asubuhi kuanzia saa 12:00.
NB: Naomba ushirikiano wa taarifa yoyote ihusuyo mwanao kwa maandishi au mdomo au kwa njia ya simu
ili kumlea vizuri mwanao na kujua wapi pa kumkazania vizuri.
Mwisho, ningependa kukukumbusha mzazi/mlezi kwamba siku ya kumtembelea mwanao ni kila jumapili ya mwisho wa mwezi.
Natanguliza shukurani zangu za dhati kwa kutuchagua na tunaomba tushirikiane katika malezi mazuri ya watoto wetu.
Nakutakieni maandalizi mazuri na karibuni sana Pandahill mpate ukamilifu.
Br. Zephania James Lusanika
Mkuu wa shule
JIMBO KATOLIKI LA MBEYA
PANDAHILL SECONDARY SCHOOL, P.O.BOX 6233, MBEYA +255755427518/ +255754459201
Kwa Mzazi/Mlezi wa ………………………………………………..
YAH: KIBALI CHA KUCHUKUA NAFASI YA KIDATO CHA V, 2016
Tunafurahi kukuarifu kwamba mtoto wako amechaguliwa kuingia kidato cha V, 2016 katika shule hii kwa mchepuo wa…………...
Unaombwa kutia sahihi yako kuthibitisha kwamba mtoto wako atachukua nafasi hii.
Karatasi hii irudishwe shuleni na itufikie kabla ya tarehe 14/06/2016. Tuma karatasi hii shuleni kwa kutumia Posta, EMS, Fax au Email
Asante,
Br. Zephania James Lusanika MKUU WA SHULE
Mimi, Mzazi/Mlezi wa …………………………………………………………………………………………………….
Nahakikisha kwamba mtoto wangu atachukua nafasi hii ya kuingia kidato cha V, 2016 kwenye shule hii hapo tarehe 16/06/2016. Niko tayari kutimiza wajibu wangu wote upande wa ada, malipo mengine na kuwa mwenye madaraka juu yake.
………………………………………… ……………………………
Tarehe Mahali
……………………………………………………. ………………………………
Jina la Mzazi/Mlezi Sahihi ya Mzazi/Mlezi
DIOCESE OF MBEYA
PANDAHILL SECONDARY SCHOOL
TEL NO: +255755427518/+255754459201 P.O. BOX 6233
MBEYA.
FAX NO: +0736607564 TANZANIA.
E-Mail:
WEBSITE: www.pandahill.org
YAH: MAELEZO YA AWALI KWA MWANAFUNZI ANAYEJIUNGA NA SHULE HII KIDATO CHA TANO - 2016.
UTANGULIZI:
Shule hii iko kilometa 25 kutoka Mbeya mjini kwenye barabara kuu iendayo Tunduma. Ipo mita 700 kutoka barabarani.
Hii ni shule ya bweni kwa wavulana na wasichana. Michepuo (subject combinations) ifundishwayo hapa ni: EGM, HKL, HGL, HGK, HGE, PCM, PGM, PCB na CBG
Shule inavyo vitabu vya kiada na ziada. Hata hivyo, mwanafunzi anashauriwa kuja na vitabu vya masomo ya mchepuo wake.
Mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni siku ya Alhamisi 16/06/2016, kuanzia saa 2.30 Asubuhi hadi saa 12.30 jioni.
MAHITAJI YA SHULE:
1. ADA
Ada ya mwaka ya masomo na hosteli kwa mwanafunzi ni Shilingi 1,600,000/= tu kwa wanaochukua masomo ya Art na Uchumi. Na Tshs 1,650,000/= kwa wanaochukua masomo ya Science (Physics, Biology na Chemistry). Ada hii inaweza kulipwa kwa awamu zisizozidi nne kama ifuatavyo:-
AWAMU / ADA / WAKATI WA KULIPAARTS / SAYANSI
I / 500,000/= / 500,000/= / Kabla ya tarehe 16 Juni, 2016
II / 500,000/= / 500,000/= / Kabla ya tarehe 08 September, 2016
III / 400,000/= / 400,000/= / Kabla ya tarehe 12 January,2017
IV / 200,000/= / 250,000/= / Kabla ya tarehe 01 April, 2017
JUMLA / 1,600,000/= / 1,650,000/=
NB: TSHS. 1,650,000/= Ni kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry na Biology)
2. MAHITAJI MENGINE
Mavazi:Sampuli za vitambaa vya sare zimeambatanishwa.
- Wavulana:
1. Suruali khaki 2.
2. Suruali nyeusi 2
3. Track suit nyekundu/blue 1 na bukta 2
4. Masharti meupe 2 mikono
mirefu.
5. Nguo za ndani
- Wasichana:
1. Sketi khaki 2 zenye marinda mengi kwa ajili ya shughuli za darasani. Urefu sm 30 toka magotini.
2. Sketi 2 nyeusi mshono wa solo, urefu 30sm toka magotini, kwa shughuli za nje.
3. Track suit nyeusi/kijivu 1
4. Mashati meupe yasiyopungua mawili mikono mirefu.
5. Doti 1 ya khanga/Kitenge
6. Nguo za ndani
(ii) Mavazi mengine kwa wote:
1. Sweta 2 kijani. (Atapewa shuleni)
2. T-shirt 2 (Atapewa shuleni)
3. Viatu vyeusi vya kamba, visigino vifupi jozi 2.(Muundo wa kawaida)
4. Soksi nyeupe jozi 2.
5. Kandambili jozi 1
6. Viatu vya michezo jozi 1.
7. Tai nyeusi 1
8. Singlet (Nyeupe) 3
9. Open shoes za kawaida
iii Vifaa vya Malazi:
1. Godoro 2 ½’ 6’ x 3”
2. Mto, foronya na chandarua.
3. Blanketi
4. Mashuka yasiyopungua mawili ya bluu
Vifaa vya usafi:
1. Beseni au ndoo
2. Vifaa vingine vya usafi wa mwili.
3. Taulo.
Vifaa vya chakula:
1 Kikombe, sahani, kijiko(vinapatikana shuleni
kwa malipo)
2 Chombo cha kutunzia maji ya kunywa lita 3 – 5. / Vifaa vya kazi:
1. Moper 1 & soft brush (Wasichana)
2. Squeezer 1& Hard brush (Wavulana)
(vinapatikana shuleni kwa malipo)
Vifaa vya Masomo:
1. Kamusi/ Dictionary
2. Penseli, karamu za rangi na karamu za wino kwa wote
3. Madaftali yasipungue 05
4. Mathematical table(Four figure).(EGM, HGE, PCM, PGM, PCB na CBG)
5. Mathematical set (Mkebe)
6. Calculator
7. Graph Pad kurasa 50.
8. Disecting kit kwa kila mmoja anayechukua somo la biologia (kama hatapata mwalimu wa biolojia atamsaidia kumnunulia)
Vifaa vingine
1. Picha 3 (Stamp size)
3. Ream 1 ya Karatasi (Photocopy paper)
4. Sanduku la Bati la kuhifadhia mali binafsi/Begi zuri na gumu linaloweza kufungwa na kuhifadhi mali binafsi.
ix Vifaa vitakavyonunuliwa hapa shuleni:
1. T-shirt 2 bei @ 12,000/=
Jumla Tshs 24,000/=
2. Sweta 2 @ 9,000/=
Jumla Tshs 18,000/=
JUMLA KUU 42,000/=
x Fedha:
1. Matumizi ya Mwanafunzi kwa robo
Muhula Tshs 40,000/=
2. Kitambulisho Tshs 4,000/=
3. Ziara za kimasomo kwa mwaka
30,000/=
JUMLA Tshs 74,000/=
xi Unadhifu na usafi
- Wanafunzi wote wanatakiwa kuwa na nywele fupi, kutokuweka dawa wala kutengeneza mtindo wowote wa nywele.- Kupaka rangi za kucha haitakiwi
- Kutinda nyusi haitakiwi
- Kufuga ndevu haitakiwi
NB: Kunyoosha nguo tunatumia pasi za umeme, hivyo mwanafunzi aweza kuja nayo au atakuwa anaazima
kwa wenzake
C. ANGALIZO:
1. Mwanafunzi ambaye atakuwa hajalipa awamu ya kwanza ya ada kwa muda uliopangwa hapo juu, ataondolewa kwenye orodha ya waliochaguliwa.
2. Malipo yote yanaweza kufanyika katika awamu moja au mbili tu kwa mtu anayetaka kufanya hivyo.
3. Vifaa vyote, isipokuwa Moper, Squeezer, Soft na Hard brush ni mali ya mwanafunzi/Mzazi aliyevigharimia.
4. Malipo ya ada na gharama za hosteli HAYATARUDISHWA kwa mlipaji endapo mwanafunzi ataiacha au atapoteza nafasi yake kwa sababu yoyote ile.
5. Malipo yote ya ada yalipwe benki ya NBC. Jina la akaunti: Diocese of Mbeya, Pandahill Secondary School. Acc. No. 016101002419. Ofisi haitapokea fedha taslimu.
6. Mwanafunzi aje na stakabadhi (Bank-pay-in slip)ya malipo ya benki, iandikwe jina la mwanafunzi mlipiwa na lengo la malipo hayo.
7. Asiye kubali nafasi aliyopewa haruhusiwi kugawa nafasi kwa mtu mwingine.
8. Mwanafunzi aje na Result slip halisi (original results slip) pia na nakala yake. Vinginevyo hatapokelewa.
9. Fedha kwa ajili ya kununulia T-shirt na Sweta, matumizi ya mwanafunzi, kitambulisho, ziara nk, ziwekwe Bank ya CRDB katika akaunti namba 01J2064081800. Jina la Akaunti: Pandahill Secondary School. Fedha ya matumizi isichanganywe na ada ya shule.
Katika risiti ya malipo ainisha malipo hayo k.m
Matumizi 40,000/=
Ziara za kimasomo 30,000/=
Kitambulisho 4,000/=
Sweta 2 18,000/=
T-shirt 2 24,000/=
Sahani 2,000/=
Kikombe 500/=
Kijiko 500/=
Moper,soft brush squeezer,hard brush,jembe&reki 10,000/=
Motisha kwa walimu 51,000/=
JUMLA KUU 180,000/=
D. MASHARTI MENGINE:
1. Vyakula vitumiwavyo hapa shuleni: ugali, wali, nyama ya ng’ombe, maharagwe, chai ya maziwa na maandazi. Matunda na mboga za majani hupatikana mara mojamoja. Bado shule haijawa na uwezo wa kuandaa na kutoa chakula cha pekee kwa wanafunzi wenye mahitaji ya pekee. (Soft diet)
2. Sare zitakazokuwa hazijashonwa istahilivyo hazitakubalika.
3. Mwanafunzi aje amevaa sare ya shule. Asije na nguo zisizotakiwa.
4. Suruali zishonwe vizuri urefu na upana wa kawaida . Zisiwe za kuburuza. Hakuna ruhusa kuvaa mlegezo. Suruali zifungwe mkanda mweusi wenye upana wa sentimeta zisizozidi 3.
5. Sketi za khaki ziwe na marinda mengi. Itavaliwa tumboni upande wa juu wa kitovu. Urefu wake upite goti kwa sentimeta 15 (6”). Marufuku kuvaa sketi kwa mlegezo.
6. Wazazi au walezi mnaruhusiwa kumtembelea mtoto Jumapili ya mwisho ya kila mwezi tangu saa 6.00 mchana – hadi saa 11:00 jioni.
7. Mwanafunzi afanyiwe uchunguzi wa afya yake na daktari anayetambulika. Daktari ajaze fomu ya afya iliyoambatanishwa.
8. Uhamisho hugharimiwa Tshs. 10,000/=
9. Ikiwa lazima, mzazi utaitwa shuleni kwa majadiliano kuhusu mwenendo wa mwanao.
10. Wanafunzi wa kiislamu waje na hijabu (wasichana), Kanzu na kofia (wavulana) kwa ajili ya sala ya Ijumaa.
11. Mwanafunzi haruhusiwi kutunza pesa chumbani. Atumie idara ya pocket money kutunza fedha zake.
12. Kila mwanafunzi anapaswa kuleta bunda (Rim) moja ya karatasi nyeupe (Photocopy paper) na hii itakuwa mara mbili kwa mwaka.
13. Mwanafunzi awe tayari kufanya mitihani au shughuli yoyote ya kimasomo siku yoyote ya juma. Kwani mwanafunzi atakayekataa kufanya mitihani au shughuli yoyote kwa sababu zozote atandolewa shuleni.
14. Soma kwa makini viambatanisho vya fomu hii (Sheria, mkataba, medical Examination form na Taarifa muhimu za mwanafunzi.
15. Mwanafunzi aje na graph paper (PAD) ambayo itamsaidia yeye mwenyewe wakati wa kujisomea hasa somo la hisabati, geogoraphia, fizikia na uchumi.
Ndimi,
Br. Zephania James Lusanika
MKUU WA SHULE
JIMBO LA MBEYA
SHULE YA SEKONDARI PANDAHILL
TARATIBU NA SHERIA ZA SHULE
(i) UTANGULIZI:
Anayekubali kuwa mwanafunzi wa shule hii, sharti akubali kuzingatia kwa makini taratibu na sheria za shule zifuatazo pamoja na sheria ndogo ndogo atakazokuwa akiambiwa.
(ii) MIPAKA YA SHULE
a) Mwanafunzi yeyote awapo shuleni haruhusiwi kwenda nje ya mipaka ya shule mpaka apate kibali kutoka kwa Mkuu wa shule au Mwalimu wa zamu.
b) Mwanafunzi anapotoka nje ya shule lazima avae sare ya shule na apite kwenye barabara kuu.
c) Maeneo waishio/walimu/wafanyakazi wasio walimu ni nje ya mipaka ya shule.
(iii) MASHARTI YA KUJALI WAKATI
Kila mwanafunzi anatakiwa kuwahi na kutenda kila kitu kwa wakati wake na mahali pake.
(iv) USAFI
a) Ni wajibu wa kila mwanafunzi kujiweka safi yeye mwenyewe na mazingira yake.
b) Ni wajibu wa mwanafunzi kushiriki kwenye shughuli za usafi wa shule
c) Kila vazi litumike katika muda na mahali kadiri ya sheria ndogo.
(v) MALI YA SHULE
a) Mwanafunzi atatakiwa kugharimia mali ya shule aliyoiharibu au kuipoteza
b) Mwanafunzi haruhusiwi kutumia moto au umeme bila idhini.
c) Ni marufuku kwa mwanafunzi kuchezea taa na kujishughulisha na nyaya za umeme.
d) Ni marufuku kwa mwanafunzi kuhamisha au kupanda darini kwa sababu yoyote ile.
(vi) BWALO LA CHAKULA
a) Ni marufuku kuingia bwaloni wakati wote usiokuwa wa chakula
b) Ni marufuku kuchukua/kuweka au kula chakula bwenini, darasani au sehemu yoyote
ile nje ya bwalo
c) Ni kosa kumpa chakula cha shule mtu asiye mwanafunzi bila idhini
d) Ni marufuku kuleta/kupokea/kununua vyakula kutoka nje ya shule (mitaani) au kutoka kwa ndugu.
(vii) VYOMBO YA MUSIKI NA MAWASILIANO:
a) Hairuhusiwi mwanafunzi kuwa na Radio/Cassette na vyombo vingine vya muziki
b) Pia mwanafunzi haruhusiwi kuwa na SIMU za mkononi atakayekutwa na simu atarudishwa nyumbani
c) Ni marufuku kwa mwanafunzi kuendesha chombo chochote cha usafiri wakati akiwa shule.
(viii) WAGENI
a) Ni marufuku kukaribisha, kumtembeza mgeni katika eneo la shule bila kupata kibali toka kwa Mkuu wa Shule au mwalimu wa zamu. Wageni wakifika wafikie utawala (mapokezi) na wapokelewe hapo.
b) Watu wafuatao tu ndiyo wataruhusiwa kumtembelea mwanafunzi: Baba, Mama au Mlezi.
(ix) MADARASANI
a) Kelele za aina yoyote darasani zinakatazwa
b) Mwanafunzi yeyote haruhusiwi kuchafua ubao, kuta, milango, dari sakafu au darasa kwa maandishi au michoro atakayethibitika atarudishwa nyumbani.
c) Wakati wowote mwalimu akiingia darasani ni lazima wanafunzi wote wasimame kwa heshima na
kumwamkia, halafu mwalimu atatoa ruhusa ya kukaa
(x) BWENINI:
a) Kelele za aina yoyote bwenini zinakatazwa
b) Ni marufuku kwa Mwanafunzi yeyote kuchemsha/kupika bwenini au kuwa na heater
c) Vyoo vyote lazima vitumiwe vizuri na kuwekwa katika hali ya usafi
d) Ni makosa kumkaribisha mgeni wa aina yeyote bwenini au katika eneo la bweni
e) Muda wa kulala na kuamka uzingatiwe kwa makini.
f) Ni marufuku kuchafua kuta, sakafu, dari, milango, madirisha n.k kwa namna yoyote ile atakayethibitika atarudishwa nyumbani.
(xi) ADHABU
a) Mwanafunzi yeyote atakayevunja sheria za shule ataadhibiwa mara moja
b) Kiranja anao uwezo wa kutoa adhabu ndogondogo kwa mwanafuzi atakayevunja sheria na taratibu za
shule. Mwalimu wa zamu apate taarifa ya adhabu hiyo kabla haijatekelezwa.
c) Kiranja haruhusiwi kutoa adhabu ya kipigo cha aina yoyote.
(xii) MAHUSIANO NA WATU WENGINE
Mwanafunzi harusiwi kufanya mazungumzo na mtu yeyote asiye mwalimu au matron katika shule bila ruhusa ya mwalimu mhusika.
Mwanafunzi haruhusiwi kutembelea, kuingia au kulala kwenye nyumba za wageni, kumbi za starehe na nyumba za wasio wazazi au walezi wake wakati yuko “mikononi” mwa shule.
(xiii) MAKOSA YANAYOADHIBIWA KWA KUFUKUZWA SHULE